Klabu ya Mashujaa Fc imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake na mshambuliaji Ismail Mgunda baada ya kufikia makubaliano na klabu ya As Vita ya Congo DRC.
As Vita inayonolewa na kocha wa zamani wa klabu ya Azam Fc Youssouph Dabo ambaye alivutiwa na mshambuliaji huyo na kuanza harakati za kumsajili ambapo walifikia makubaliano binafsi na mchezaji huyo huku ikibaki kumalizana na timu yake.
Mgunda alibakisha mkataba wa mwaka mmoja na nusu na wazee wa mapigo na mwendo sasa ni mali ya AS vita baada ya dili hilo kukamilika kwa klabu hizo kufikia makubaliano.
Mgunda mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Jomo Cosmos ya nchini Afrika ya kusini pamoja na vilabu vya Ruvu Shooting na Singida United Fc ana mwili mkubwa wenye misuli ambayo huwasumbua mabeki wa timu pinzani sambamba na uwezo wake wa kasi pamoja na kufunga.
Kocha Yousouph Dabo ameona kuwa mshambuliaji huyo ataisaidia klabu yake katika ligi kuu ya nchini Dr Congo.