Mshambuliaji wa zamani wa Toto Africans ya Mwanza na Azam Fc Waziri Junior amejiunga na timu ya Mbao fc ya jijini Mwanza kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Waziri aliibukia Toto Afrika ya Mwanza na kisha alisajililiwa na Azam fc japo hakupata nafasi ya kucheza kutokana na kukabiliwa na majeraha ya mara kwa mara mpaka alipotolewa kwa mkopo na matajiri hao wa chamazi.
Waziri mwenye uwezo wa kucheza kwa ufasaha nafasi za ushambuliaji wa kati atajiunga na timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa kliniki ya michezo ya timu hiyo ya kutafuta vipaji inayofanyika katika uwanja wa Ccm Kirumba.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.