Home Makala Stars Kuwavaa Burundi Kombe la Dunia

Stars Kuwavaa Burundi Kombe la Dunia

by Dennis Msotwa
0 comments

Timu ya taifa ya Tanzania(Taifa stars) itavaana na Burundi (The amavubi) katika michezo ya awali ya kutafuta nafasi ya kufuzu kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Ratiba hiyo iliyotolewa na shirikisho la soka barani Afrika (Caf) inaonyesha Stars itavaana na amavubi kati ya tarehe 2 mwezi wa tisa na marudiano itakua tarehe 9 mwezi huo huo.

Ratiba hiyo imetoka kwa kuzingatia viwango vya nchi vya mwezi juni kama vilitolewa Shirikisho la soka duniani(Fifa) ambapo kwa Afrika timu zilizoshika nafasi 26 za juu hazitoanza katika hatua za awali bali itasubiri matokea ya timu 28 ambazo zimeanza hatua za awali ambapo timu 14 zitasoka mbele na kuungana na zile 26 kutengeneza makundi.

banner

Timu hizo zitawekwa kwenye makundi 10 ya timu nne na kumi zitakazoongoza makundi hayo zitapangiwa ratiba ya mtoano ili kupata timu tano zitakazofuzu kwenda nchini Qatar ambapo katika fainali zilizopita nchini Urusi Afrika iliwakilishwa na timu za Nigeria,Senegal,Morroco,Misri na Tunisia.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited