Katika kuendelea kukisuka kikosi chao kuelekea msimu ujao wa ligi kuu ya Nbc na michuano ya kimataifa nchini,Klabu ya Azam Fc imewatambulisha mastaa wawili kikosini humo kuja kuongeza nguvu katika kikosi hicho ikiwa ni mapendekezo ya kocha Frolent Ibenge ambaye ametua klabuni hapo msimu huu.
Azam Fc imemtambulisha winga Ihmid Baraket kutoka katika klabu ya Cs Sfaxien ya nchini Tunisia ambaye imemsajili kwa mkataba wa miaka miwili ili kuleta makali katika safu ya kiungo ya klabu hiyo ambapo katika tathmini fupi ya kocha Ibenge katika wiki mbili za kambi ya klabu hiyo wilayani Karatu mkoani Manyara ameona kuwa anamhitaji winga huyo.
Pia Ibenge amesamjili staa mwingine Ben Zitoun Tayeb ambaye ni mshambulaiji wa kati huku pia akiwa na uwezo wa kucheza nafasi ya beki wa kati akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na klabu ya Al Hilal Fc iliyokua chini ya Ibenge kabla ya kujiunga na Azam Fc.
Baraket ana uwezo wa kucheza nafasi za kiungo zote za ushambuliaji akitumia mguu wa kushoto akiweza kutokea kulia ama kushoto pamoja na mshambuliaji wa pili ama namba kumi ambapo aliweza kuonyesha uwezo mkubwa sana katika klabu hiyo ya Cs Sfaxien nchini Tunisia.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ibenge hajaridhishwa na mawinga aliowakuta klabuni hapo ambapo alihitaji winga mwingine wa kusaidiana na Idd Nado baada ya Gibril Sillah kuondoka klabuni hapo baada ya kupata ofa nene katika nchi za kaskazini Es Setif ya nchini Tunisia,
Msimu Azam Fc ni kama imeamua baada ya kufanya usajili mzito kuanzia benchi la ufundi mpaka wachezaji wa ndani ambao imesajili mastaa wenye uzoefu mkubwa katika michuano mbalimbali ikilenga kufanya vizuri katika michuano ya ndani na ile ya kimataifa ambapo pia imefanikiwa kumbakisha kiungo mshambuliaji Feisal Salum ambaye ilidaiwa anajiunga na Simba Sc.
Aishi Manula,Edward Charles Manyama,Himid Mao Mkami ni moja ya sajili za wachezaji wazoefu ambao walikulia klabuni hapo lakini wamerudishwa kuja kuongoza jahazi la klabu hiyo kupambania ubingwa msimu huu.