Home Makala Mghana Wa Yanga Atoa Tamko

Mghana Wa Yanga Atoa Tamko

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji mpya wa Yanga aliye sajiliwa dakika za mwisho kabla ya usajili wa dirisha dogo kufungwa ,Benard Morrinson raia wa Ghana amewaondoa hofu wanayanga kwa kuwaambia tatizo limeisha kwa upande wa ushambuliaji kwa kuwa tayari ameshatua yeye.

Benard Morrinson alisema kuwa amekuja amekuja Yanga kwa ajili ya kufanya kazi baada ya kuona kwenye upande wa ushambuliaji kuna tatizo hivyo atatumia nafasi atakayoipata kufunga na kutengeneza nafasi kwa wachezaji wenzake nao waweze kufunga.

“Ninaamini hadi viongozi wamefikia hatua ya kunisajili ni baada ya kuona kuna tatizo la ushambuliaji katika timu, ninaamini kama lisingekuwepo hilo basi nisingekuwa hapa, hivyo niahidi kuifungia Yanga mabao,” alisema Morrison aliyewahi kuzichezea Orlando Pirates na Motema Pembe.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited