Kiungo wa Arsenal,Mesut Ozil ameonyesha utu wa kuwajali wengine baada ya hivi karibuni kutoa kiasi cha pauni 80,000 (sh milioni 231) kwa lengo la kuwasaidia waislamu ambao wameathirika na janga la virusi vya Corona katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani.
Nyota huyo ambaye ni raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki atasaidia chakula kwa ajili ya Waislamu 16,000 kwa kipindi chote cha mwezi wa Ramadhan ulioanza April kwa kusaidia kufuturisha maeneo magumu ya nchini Uturuki.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ozil anapokea mkwanja mrefu ndani ya Arsenal , ambao ni pauni 350,000 pia amekuwa ni mtoaji mzuri kwani amekuwa akiwalisha watu 100,000 wasio na makazi.