Klabu ya Mbao fc imeibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-o dhidi ya polisi Tanzania mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa katika uwanja wa Ccm Kirumba.
Bao la mbao lilifungwa na Waziri Junior dakika ya 65 na lilidumu mpaka mwisho mwa mchezo na kuifanya Mbao fc kuchukua pointi 3 muhimu japo hazikutosha kuinyanyua katika msimamo wa ligi kuu ambapo imesalia nafasi ya 19 ikiwa na pointi 29 katika michezo 32.
Huu ni mchezo wa pili mfululizo kwa mbao kuibuka na ushindi chini ya kocha Felix Minziro ambapo awali waliifunga Coastal Union bao 1-0.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.