Ikiwa imesalia michezo miwili kumalizika kwa ligi ya La liga,Klabu ya Real Madrid inahitaji kushinda mchezo ujao ili kutangazwa mabingwa wa ligi hiyo baada ya jana kufanikiwa kuwafunga Granada mabao 2-1.
Mabao ya Ferland Mendy na Karim Benzema yalitosha kuwahakikishia alama tatu muhimu vijana hao wa Zinedine Zidane hivyo kuhitaji alama tatu tu ili kutangazwa mabingwa wa ligi hiyo.
Real Madrid itawavaa Villareal siku ya Alhamis pamoja na Leganes siku ya jumapili na wakishinda mchezo mmojawapo au kutoa sare michezo yote watakua mabingwa wa ligi hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.