Siku ya Simba Day wanamsimbazi watasherekea wakiwa uwanja wa Mkapa wakitazama mchezo mkali kati ya Simba Sc na Vital’O ya Burundi siku ya Agosti 22,2020.
Simba Sc imethibitisha kucheza na waburundi hao kupitia ukurasa wao wa instagram huku kabla ya mchezo huo Simba itatangulia kuwatambulisha wachezaji wake watakaoitumikia klabu hiyo kwenye msimu 2020/2021 na ligi ya mabingwa Afrika.
Mpaka sasa timu hiyo imeshasajili wachezaji nane wakiwa ni Benard Morrison,Charles Ilanfya,David Kameta,Joash Onyango,Chris Mugalu,Larry Bwalya na Ibrahim Ame.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.