Uongozi wa Simba Sc umesema kuwa Luis Miqussone’Konde Boy’ bado hajarejea bongo kwa ajili ya maandalizi ya ligi kwa sababu aliomba ruhusa aende akaoe.
Luis amekuwa bora msimu wa kwanza akitupia jumla ya mabao matano na pasi mbili za mabao kwenye mashindano yote ikiwa ni kombe la shirikisho alitupia mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao huku ligi kuu bara ametupia mabao matatu na pasi moja.
Taarifa hiyo imethibitishwa na ofisa habari wa Simba, Haji Manara ambaye amesema kuwa baada ya ligi kuu kuisha na mchezo wa kombe la shirikisho, Luis aliomba ruhusa akaoe kwani ni jambo la msingi kwake.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.