Wolves, Newcastle na Everton ni miongoni mwa vikosi zinavyowania saini ya beki wa Arsenal Maitland-Niles ambaye anatazamiwa kuondoka Emirates mwishoni mwa Agosti, 2020.
Beki huyo ambaye pia ni mzaliwa wa Uingereza ameitumikia Arsenal katika jumla ya mechi 32 za mapambano yote ya msimu wa 2019-20 na amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kilichowachapa Chelsea 2-1 kwenye fainali ya Kombe la FA iliyochezewa katka uwanja wa Wembley, Uingereza mnamo Agosti 1, 2020.
Arsenal wanapania kujisuka upya msimu wa 2020/2021 na tayari wamemtia Maitland-Niles mnadani tayari kwa kusajiliwa na klabu yoyote itayoweza kutoa thamani ya pesa itakayowekwa mezani.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.