Yanga Sc ipo kwenye harakati za kufanya vizuri msimu wa pili wa ligi kuu bara,hivyo hata mabadiliko ya sehemu ya kufanyia mazoezi na makazi yao wamebidi kuyaboresha ili kujenga utulivu zaidi kwa ajili ya msimu wa 2020/2021.
Kambi hiyo ya Yanga iliyopo jijini Dar-es-salaam imejificha Kigamboni katika kijiji cha Maraha ,Avic Town na kimetawaliwa na viwanja vizuri wa kufanyia mazoezi mbalimbali pamoja na appartment za kupumzikia baada ya mazoezi.
Wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Yanga Sc wanafarijika na mazingira ya kambi hiyo mpya kwani ni rafiki kwao katika maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu bara inayoanza Jumapili ya Septemba 6,2020.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.