Simba Sc wamelifungua vyema pazia la Ligi kuu bara baada ya kunyakua pointi tau kutoka kwa Ihefa Fc iliyoburuzwa kwa mabao 2-1.
John Bocco ambaye ni nahodha wa klabu hiyo ameanza kuwapatia Simba Sc bao la kwanza dakika ya pili ambapo lilisawazishwa na mchezaji wa Ihefa Fc,Omary Mponda dakika ya 15.
Bao la lililowapa ushindi Simba lilipachikwa na Mzamiru Yassini dakika ya 42 ambalo lilidumu dakika 90 za mchezo na kuwafanya wanamsimbazi hao kuanza msimu vizuri kwa kunyakua pointi tatu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Ihefu fc imepanda daraja msimu huu na imewapa tabu mabingwa watetezi Simba leo kwani wanacheza soka la utulivu na kwa umakini mkubwa .