100
Miongoni mwa dili ambalo limezungumzwa kwa muda wote na halijaonesha mafanikio ndani ya Manchester united ni la Jadon Sancho ambaye ameifungia Borrusia Dortmund jumla ya mabao 20 msimu uliopita na kutoa pasi 20 kwenye mashindano yote.
Manchester United bado wana imani kuwa watamsajili Sancho ambaye ni chaguo la kwanza la kocha mkuu wa klabu hiyo,Ole Gunnar Solskajaer kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Kwa mujibu wa ripoti ya Dagbladet ,Solskjaer amemwambia nyota huyo wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho kuwa dili lake la kujiunga na United litakamilika hivi karibuni.
Mpaka sasa United walishindwa kutoa fedha ya pauni milioni 108 ambayo Dortumund wanahitaji ili wamuachie kiungo Sancho mwenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.