Baba mzazi wa staa anayeichezea As Roma,Francesco Totti,Enzo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76 baada yakupata shambulio la moyo miaka michache iliyopita huku akikumbwa na corona iliyomuweka katika orodha ya watu waliopo kwenye hatari zaidi ya kutonusurika kupona.
Mzawa huyo wa Italia,Enzo alipenda kuhudhulia mechi zote za As Roma popote walipokuwa wakienda huku akijitolewa kuwapelekea wachezaji hao Pizza wakiwa mazoezini kwaajili ya kuwatia moyo kwani alikuwa anapenda sana soka ambalo mwanaye alichagua kulitumikia.
Mzazi huyo wa Totti amefariki katika hospitali ya Lazzaro Spallanzani iliyopo Rome akiiacha mke na watoto wawili ambao ni Francesco na Riccardo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
As Roma imeonekana kuguswa na kifo hicho cha baba mzazi wa Totti hata kukitangaza kupitia mitandao yao ya kijamii huku ikitoa pole zao za dhati kwa familia ya marehemu ikiwepo mke wake,Fiorella na watoto wake,Francesco na Riccardo pamoja na ndugu wote jamaa na marafiki.