Klabu ya Tp mazembe imeanza kuwafatilia mastaa wawili wa klabu ya Yanga sc Bakari Mwamnyeto na Feisal Salum ili kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao.
Wachezaji hao ambao wamekua na uhakika wa namba katika klabu ya Yanga sc wamewashawishi matajiri hao kutoka Kongo na inadaiwa watatumia michezo miwili ya michuano ya kimataifa kufuzu Afcon 2021 dhidi ya Tunisia kuwaangalia zaidi.
Mwamnyeto alijiunga na Yanga sc msimu huu akitokea Coastal Union Fc kwa mkataba wa miaka miwili huku Feisal akiwa bado na mkataba mrefu wa miaka minne na timu hiyo ya Jangwani Kariakoo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.