Home Soka Ibenge Arejeshwa Drc Congo

Ibenge Arejeshwa Drc Congo

by Sports Leo
0 comments

Kocha huyo Mkuu wa Klabu ya AS Vita Club ya Nchini Congo Frolent Ibenge ameteuliwa kuiongoza timu ya taifa ya Congo Katika Michuano ya CHAN inayotarajiwa kufanyika huko Nchini Cameroon kutoka Januari 16 hadi Februari 7, 2021.

Ibenge ambaye Alikuwa Kocha wa DR Congo Katika Mashindano yote Kutoka 2014 Hadi 2019 nafasi yake ikichukuliwa na Christian Nsengi-Biembe,Amerejea katika timu ya Taifa hilo na atasaidiwa na Pamphile Mihayo kocha wa Tp Mazembe na Daula Lopembe huku Kocha wa makipa akiwa ni Eugène Bulayima.

DRC itaanza Michuano hiyo kwa Mechi ya Congo derby Dhidi ya Congo Republic Katika dimba la Japoma stadium mjini Douala – DRC ambao ndio Mabingwa Mara mbili wa Mashindano wapo Kundi B pamoja na Niger na Libya.

banner

Ikumbukwe Ibenge aliiongoza DRC Kuwa Mabingwa wa Michuano hii huko Rwanda mwaka 2016.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited