Klabu ya Namungo imekamilisha usajili wa Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Olympic Star ya nchini Burundi Kwizera Eric maarufu kama Messi wa Burundi ili kuisadia katika mbio za ubingwa wa ligi kuu na michuano ya kimataifa.
Mshambuliaji huyo anayemudu kukatiza mbele ya msitu wa mabeki ataanza kuitumikia Namungo Fc kwenye mashindano ya Mapinduzi cup yanatarajiwa kuanza siku ya kesho huko Zanzibar.
Eric Kwizera ana mudu vizuri kucheza namba 7,9,10 na 11 na anatarajiwa kutoa changamoto kwa mawinga wa klabu hiyo Shiza Kichuya,Idd Kipagwile na wengine.