Mashabiki wa klabu ya Simba sc wamelilia benchi la ufundi la klabu hiyo linaloongozwa na Didier Gomez na Selemani Matola baada ya jana safu hiyo kuruhusu mabao mawili dhidi ya Azam Fc katika mchezo ulioisha kwa sare ya 2-2.
Mashabiki hao walilalamika safu ya kiungo cha ulinzi na beki iliyokua chini ya Thadeo Lwanga pamoja na Serge Pascal Wawa kuzembea kiasi cha kuruhusu bao la kwanza lililofungwa na Idd Selemani ambaye alisawazisha bao la Meddie Kagere huku pia akitumia uzembe wa mabeki wa Simba sc kutoa pasi ya bao kwa Ayoub Lyanga aliyefunga bao la pili.
Licha ya safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo kukosa mabao matatu ya wazi lakini juhudi ya binafsi za Luis Miqquissone zilisaidia Simba sc kusawazisha bao la pili na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kutokana na matokeo hayo Simba sc amesalia katika nafasi ya pili ya msimamo akiwa na alama 38 huku Yanga sc wakiwa kileleni na alama 43 japo Simba sc wana mchezo mkononi.