Ikiwa tayari yamesalia masaa machache kucheza mchezo wa kwanza wa robo fainali baina ya Kaizer Chiefs dhidi ya Simba sc utakaofanyika katika uwanja wa Fnb Stadium tayari wasauzi hao wamepata kiwewe kutokana na ubora wa Simba sc.
Licha ya kwamba wapo nyumbani timu hiyo imeingia na kiwewe kufuatia kuwa na mwenendo wa kusuasua huku wakitoa sare katika mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu nchini humo hali iliyowalazimisha mashabiki wa klabu hiyo kuandamana wakishinikiza matokeo bora na mabadiliko makubwa ya timu.
Ugumu wa mchezo huo unachagizwa pia na ubora wa Simba sc wanapokua nyumbani hivyo kuwalazimu kaizer kuhakikisha wanapata matokeo katika mchezo wa leo kabla ya ule wa marudiano utakaofanyika Dar es salaam.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.