Klabu ya Simba sc imeruhusu kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Kaizer Chiefs Fc katika mchezo wa robo fainali ya klabu bingwa barani Afrika uliofanyika katika uwanja wa Fnb stadium jijini Johanersburg nchini humo.
Simba sc iliruhusu bao la mapema dakika ya sita ya mchezo lililofungwa na Erick Mathoho kwa kichwa akimalizia mpira wa kona huku Samir Nurkovic akifunga pia dakika za 34 na 57 kwa kichwa na msumari wa mwisho ukifungwa na Leonardo Castro dakika ya 63 amabao yaliyodumu mpaka mwisho wa mchezo.
Simba sc sasa watakua na kibarua kigumu cha kusawazisha matokeo hayo wikiendi ijayo watakaporudiana jijinin Dar es salaam.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.