Home Soka Okwi Atoweka,Simba sc Watajwa

Okwi Atoweka,Simba sc Watajwa

by Sports Leo
0 comments

Nyota wa klabu ya Al Itihad FC ya Misri na staa wa zamani wa Klabu ya Simba, Emmanuel Okwi inaelezwa kuwa hayupo kwenye kambi ya Al Itihad kwa muda wa mwezi sasa.
Raia huyo wa Uganda ambaye ni nahodha pia wa timu ya Uganda, Okwi inaelezwa kuwa yupo kimya mpaka sasa kuhusu kurejea kambini.

Kwa mujibu wa tovuti ya Korabia.Com ya nchini Misri ilimnukuu Rais wa Klabu ya Al Ittihad, Mohamed Mousely baada ya mchezo wa timu hiyo dhidi ya Ismaily wakishinda 2-1.

Mohamed alisema:”Kuna wachezaji akiwemo Okwi hawapo kambini, wametoroka kwani tumewatumia barua lakini bado kimya, walikwenda kwenye timu zao za taifa lakini hawajarudi hadi sasa,”.

banner

Ripoti nyingine zilidai kuwa Okwi ameamua kutorejea kwenye klabu yake hiyo kwa kuwa mkataba wake ulimalizika Juni 31 mwaka huu na hakukuwa na mazungumzo ya kumuongezea dili jipya.

Okwi amefanikiwa kufunga mabao matatu katika mechi 17 alizocheza ndani ya msimu huu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited