Kiungo wa Kimataifa wa England na klabu ya Aston Villa Jacky Grealish anakaribia kujiunga na klabu ya Man city mara baada ya vilabu hivyo kufikia hatua za mwisho za makubaliano.
Aston Villa wapo tayari kupokea ofa ya Man city ya paundi milionoi 100 na tayari imeshawasajiri Leone Bailey na Danny Ings kama hatua za kujiandaa na maisha bila ya nahodha wao huyo.
Grealish tayari yupoj jijini Manchester na atarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na kutambulishwa rasmi ndani ya wiki hii.Usajili huu utakuwa ghali zaidi katika historia ya soka ya England ukiupiku ule wa Pogba kwenda Man Utd kwa paundi milioni 89 akitokea Juventus.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.