Beki kitasa wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Henoc Inonga Baka amejiunga na mabingwa wa soka Tanzania klabu ya soka ya Simba akitokea DC Motema Pembe akiwa mchezaji huru.
Henoc ni moja kati ya mabeki mahiri katika ligi ya DRC na mara kwa mara amekuwa akiitwa timu ya taifa hilo huku uchezaji wake ukifananishwa na beki wa Kifaransa Rafael Varane anayeichezea Man Utd ya Uingereza.
Kitasa hicho kinaenda kuweka ushindani mkubwa wa namba kwa mabeki Pascal Wawa na Joash Onyango ambao wamejihakikishia namba za kudumu katika kikosi cha Simba.