Home Makala Simba sc 2-2 Far Rabat

Simba sc 2-2 Far Rabat

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Simba sc iefanikiwa kuibuka na sare ya mabao 2-2 dhidi ya timu ya Far Rabat ya Morroco katika mchezo wa maandalizi ya msimu mpya ambapo klabu hiyo imeweka kambi nchini humo.

Simba sc ilivaana na timu hiyo inayonolewa na kocha wa zamani wa klabu hiyo Sven Vandebroek ambapo mpaka mapumziko Simba sc ilikua nyuma kwa mabao 2 kwa bila lakini kuingia kwa Hassan Dilunga kulifanikiwa kubadili ubao wa matokeo baada ya mchezaji huyo kuiwahi pasi ya haraka kutoka kwa Ibrahim Ajibu na kufunga bao dakika ya 54.

Wakati mchezo ukiwa ukingoni ulipigwa mpira mrefu na mabeki wa Simba sc ambao ulimkuta Jimson Mwinuke alimpa pasi mfungaji Pape Sakho aliyefunga bao la kusawazisha nakufanya ubao usomeke 2-2 mpaka dakika ya mwisho ya mchezo.

banner

Simba sc bado inaendelea na kambi hiyo huku ikiratarajiwa kucheza michezo mingine ya kirafiki kabla ya kurejea nchini kujiandaa na mchezo wa ngao ya Hisani dhidi ya Yanga sc utakaofanyika Septemba 25.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited