Aliyekua msemaji wa klabu ya Simba sc Haji Manara ameendelea kurusha vijembe kwa mabosi wake wa zamani baada ya kuhamia katika klabu ya Yanga sc kama msemaji mpya wa klabu hiyo akiungana na Hassan Bumbuli na Antonio Nugaz.
Haji wakati wa utambulisho wake katika klabu ya Yanga sc alilisisitiza kuwa amejiunga na mabingwa wa kihistoria na mabingwa mara 27 wa ligi kuu huku akisema kuwa Yanga sc ni timu kubwa hapa nchini.
Msemaji huyo ambaye alikua Mc katika tukio la uzinduzi wa jezi za Yanga sc ambapo alitupa kijembe wa waajiri wake wa zamani kuwa timu hiyo imezindua jezi na sio makorokoko akimaanisha kuwa jezi hiyo haina matangazo mengi ya biashara za kampuni fulani.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Yanga sc imezindua jezi za aina tofautitofauti kwa ajili ya mechi za nyumbani na ugenini huku pia kukiwa na jezi za kusafiria na jezi za mashabiki ambazo tayari zimeanza kuuzwa mtaani na katika maduka ya Gsm nchini.