Aliyekua kipa wa klabu ya Yanga sc Farouk Shikhalo amejiunga na klabu ya klabu ya Kmc kwa mkataba wa mwaka mmoja akiwa kama mchezaji huru baaada ya kutoongeza mkataba na klabu ya Yanga sc aliyoitumikia kwa miaka miwili.
Kipa huyo raia wa Kenya alitua nchini miaka miwili iliyopita akitokea Bandari Fc ya kenya ambapo alifanikiwa kuwa kipa bora wa msimu huo na akajiunga na Yanga sc ambapo hakuwa na namba ya uhakika bali walipokezana na Metacha Mnata ambao mwishoni walitemwa wote kwa mapendekezo ya kocha Nasredine Nabi.
Shikhalo aliyekua kipenzi cha mashabiki wa klabu ya Yanga sc atakua na jukumu la kutafuta nafasi mbele ya Juma Kaseja aliyedumu Kmc huku akitumika kama kipa chaguo la kwanza kwa misimu kadhaa sasa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.