Home Soka Wabrazil kuikosa EPL wikiendi hii

Wabrazil kuikosa EPL wikiendi hii

by Dennis Msotwa
0 comments

Chama cha soka cha Brazil kimeliomba shirikisho la soka duniani (FIFA) kuwazuia wachezaji wa vilabu vya EPL kucheza michezo miwili mmoja wa EPL na mwingine wa ligi ya mabingwa Ulaya ambao timu zao ziliwazuia kujiunga na timu ya taifa hiyo kwenye michezo ya kufuzu kombe la dunia Qatar 2022.

Wachezaji hao ni pamoja na magolikipa wa Liverpool na Manchester city Alison Becker na Ederson wengine kiungo wa Manchester United Fred,kiungo wa Liverpool Fabinho na beki wa Chelsea Thiago Silva na washambuliaji Firmino wa Liverpool,Gabriel Jesus wa Man city na Raphina wa Leeds United.

Vilabu vikubwa vya EPL viliwazuia wachezaji wake kadhaa hasa wale kutoka timu za Amerika ya Kusini kujiunga na timu zao za taifa kukwepa kuwekwa karantini ya siku kumi pindi watakaporejea England.

banner

Mataifa kama Brazil,Argentina na Uruguay yapo kwenye mstari mwekundu kuingia Uingereza kutokana na hali ya Uviko-19 na vikwazo vya kusafiri baina ya mataifa hayo.

Kwa mujibu wa sheria za FIFA ni kosa kwa vilabu kuzuia wachezaji wake kutumikia mataifa yao katika michezo mbalimbali inayotambulika na shirikisho hilo.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited