Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameambiwa na mashabiki wa klabu hiyo kuwa anatakiwa abakie kufanya majukumu yake ya kuifunza timu badala ya kuingilia na kuwaambia mashabiki nini cha kufanya.
Pep alilamika uchache wa mashabiki wa timu hiyo walijojitokeza kushuhudia mchezo wa michuano ya klabu bingwa Ulaya kwenye mkutano na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo huo dhidi ya RB Leipzig walioshinda 6-3.
Mkufunzi huyo alisema kuwa mashabiki wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Southampton kwani wamefunga mabao 16 katika michezo mitatu hapo Etihad hivyo mashabiki wanapaswa kuhamasika,akionesha kutoridhishwa na mahudhurio.
Katika wa klabu ya mashabiki wa Man City alisema ”Pep ni kocha bora duniani nadhani anatakiwa kubakikuwa hivyo,haelewi ugumu ambao mashabiki wanaweza kuwa wanapitia katika dimba la Etihad hasa mechi za katikati ya juma.Wana watoto kuwahudumia wakati mwingine hawawezi kumudu gharama za tiketi.Lakini pia kuna maswala ya Uviko-19 hivyo sielewi kwanini analalamika”.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Guardiola amekuwa akilalamika kukosekana kwa hamasa ya mashabiki wa Man City kuhudhuria na kuipa nguvu timu hiyo hwaswa kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya.