Home Soka OMOG kocha mpya Mtibwa

OMOG kocha mpya Mtibwa

by Sports Leo
0 comments

Kocha wa zamani wa vilabu vya Azam FC na Simba SC Joseph Omog ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa wakati miwa wa Manungu Turiani mkoani Morogoro klabu ya Mtibwa Sugar.

Mcameroon huyo aliipa mafanikio ya kuchukua ubingwa klabu ya Azam FC msimu wa 2012/2013 bila kupoteza hata mchezo mmoja,na ndio ubingwa pekee iliyowahi kuupata tangu kuanzishwa na kupanda ligi kuu soka Bara mwaka 2008.

Baada ya mafanikio yake Azam mkufunzi huyo aliwavutia mabingwa wa ligi kuu Simba SC na kujiunga nayo mwaka 2016 ambapo aliiwezesha kupigania ubingwa mpaka dakika za mechi ya mwisho ambapo waliukosa kwa tofauti ya magoli.

banner

Mtwiba Sugar ilikua imeshaanza kunolewa na Mrwanda Thiery Hitimana ambaye dakika za mwisho aliwakacha baada ya kupokea mkataba mnono kutoka Simba.

Kocha huyo amesindikizwa na msafara wa magari kumi kwenda Makao makuu ya klabu hiyo Manungu Morogoro mara baada ya kupokelewa kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Juliu Nyerere.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited