Kocha wa zamani wa Chelsea na Leicester Claudio Ranieri amekubali kimsingi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Watford inayoshiriki ligi kuu soka nchini Uingereza akichukua nafasi ya Xisco Munoz aliyefutwa kazi.
Watford ilifikia maamuzi ya kumfukuza kocha wao Mhispania Xisco mara baada ya kupoteza kwa 1-0 dhidi ya Leeds United kwenye mchezo wa ligi siku ya Jumamosi kutokana na muendelezo mbaya wa matokeo kwa kushinda mechi mbili tu baada ya mechi saba iliyocheza timu hiyo.
Ranieri(70) aliingoza Leicester city kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka Uingereza mwaka 2016 na baada ya kuondoka Leicester alijunga na As Roma kabla ya kutimuliwa na kutua Sampdoria ambayo aliacha nayo mwako 2020.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Xisco Munoz amekuwa kocha wa kwanza kufukuzwa msimu huu kwenye ligi hiyo huku makocha wengine kama Dani Farke wa Norwich,Steve Bruce wa Newcastle,Ole Gunnar Solskjaer wa Man Utd na Mikel Arteta wakitajwa kuwa huenda wakafuata katika kadhia hiyo.