Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Paris Saint German amekiambia kituo cha habari za michezo cha RMC cha nchi hiyo kuwa ni kweli aliomba kuondoka klabuni hapo katika dirisha lililopita la usajili la majira ya joto.
Mbappe amesema kuwa aliomba kuondoka mwezi Julai mwaka huu kwasababu kwa kipindi hicho hakutaka kuongeza mkataba mpya wa kuendelea na matajiri hao,hivyo alitaka PSG wapate ada ya uhamisho ili waweze kupata mbadala wake sahihi atakapoondoka.
Aliendelea kusema ”nilitaka kutovunjiana heshima kati yangu na klabu,nikawaambia kama hamtaki niondoke basi sawa nitasalia hapa.Binafsi sikufurahishwa na PSG kusema kuwa nimeomba kuondoka ndani ya wiki ya mwisho ya mwezi Agosti kwasababu si kweli,ilinifanya nijisikie kama mwizi,niliwaambia mapema mwezi Julai na sio kama walivyosema”.
Mchezaji huyo pia amepinga madai kwamba alikataa ofa 7 za kuongeza mkataba kutoka PSG akisema kuwa amekuwa na furaha kwa misimu minne yote aliyoitumikia timu na bado ana furaha licha ya kushindwa kuondoka.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mbappe anatarajiwa kuondoka bure PSG na kujiunga na Real Madrid ambao ndio klabu pekee iliyoonesha kumhitaji katika dirisha lililopita la usajili.