Klabu ya Newcastle United imemtangaza kocha wa zamani wa AFC Bournemouth Eddie Howe kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo akisaini mkataba utakaomuweka St James Park hadi majira ya joto mwaka 2024.
Howe amechukua mikoba ya Muingereza mwenzake Steve Bruce aliyefukuzwa kazi mwezi Oktoba kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyo kwenye ligi kuu ya Uingereza ikiwa haijashinda hata mchezo mmoja.
Eddie alikuwa aliipandisha Bournemouth kwenye ligi hiyo mwaka 2015 huku ikicheza soka zuri la kushambuliaji lililoifanya watu wengi kuvutiwa kuiangalia timu hiyo ikicheza,japo ilishuka daraja mwaka 2020 na kuamua kuachana nayo.
Kazi kubwa kwa mkufunzi huyo kwasasa ni kuhakikisha timu hiyo inasalia kwenye ligi huku ujenzi wa timu hiyo ukiendelea kupitia maingizo ya wachezaji kuanzia dirisha la usajili la Januari,kazi yake imekuja wakati sahihi wa kipindi hiki cha mechi za kimataifa hali ambayo itamsaidia kuzoeana na kurudisha hali ya upambanaji kwa wachezaji wake ambao wengi hawazitumikii timu zao za Taifa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mmoja ya wamiliki wa klabu hiyo Amanda Staveley amesema kuwa ”Eddie ni mtu sahihi kwa kile wanachotaka kukijenga,wanayo furaha kumkribisha yeye na wenzie St James’ Park na wanaangalia mbele kufanya kazi pamoja kufikia malengo waliyojiwekea.
Eddie mwenyewe amesema kuwa ”nina furaha kupata fursa hii,ingawa kuna kazi kubwa sana ya kufanya,nina hamu ya kuingia viwanja vya mazoezi na kuanza safari hii na kufanya kazi na wachezaji wangu.