Mwanariadha maarufu duniani kutoka Jamaica amesema kuwa anasikitishwa sana na kocha Antonio Conte kujiunga na Tottenham Hotspurs ya Uingereza kwani alitamani sana kocha huyo kutua Man United.
Bolt ni shabiki mkubwa sana wa mashetani wekundu Man Utd na mara kwa mara amekuwa akihudhuria michezo ya nyumbani ya timu hiyo na mara kwa mara amekuwa akionesha hisia zake kwa klabu hiyo kupitia mitandao yake ya kijamii.
Akihojia na skysports Bolt amesema kuwa Conte ni kocha mshindi na mwenye uwezo mkubwa sana wa kufundisha soka,amethibitisha hilo kila alipokwenda kwa kutwaa mataji na kama angetua Old Trafford basi angeirejesha klabu yake kwenye zama za mataji.
Aliendelea kusema kuwa hongera kwa Spurs kumpata kocha huyo kwani ataiunganisha timu hiyo na kuifanya kuwa moja ya timu tishio barani Ulaya endapo watamtimizia mahitaji yake.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kauli ya mwanariadha huyo anayeshikiria rekodi mbalimbali za dunia kwenye riadha inaonesha kuwa hana imani tena na kocha Ole Gunnar Solskjaer ambaye yupo kwenye shinikizo la kufukuzwa.