Home Soka Man Utd Yaamka Yaipiga Villareal

Man Utd Yaamka Yaipiga Villareal

by Dennis Msotwa
0 comments

Baada ya kupitia kipindi kigumu katika michezo mbalimbali ya ligi kuu nchini Uingereza hatimaye klabu ya Manchester United imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Villareal inayonolewa na kocha Unai Emiry katika mchezo wa ligi ya klabu bingwa barani ulaya.

United inayonolewa na kocha wa muda Michael Carrick haina budi kumshukuru Kipa David De Gea ambaye aliokoa hatari kadhaa langoni kutokana na safu ya ulinzi ya Manchester United kujichanganya mara kwa mara.

Kuingia kwa Bruno Fernandes aliyechukua nafasi ya Donny Van de Beek kuliongeza spidi ya kukaba kuanzia mbele na kuipa presha safu ya ulinzi ya Villareal na kufanikiwa kupata bao la kuongozwa lililofungwa na Cristiano Ronaldo 78′ huku Jadon Sancho akifunga bao lake la pili dakika ya 89′ na kuipa ushindi United huku ikifanikiwa kuongoza  kundi hilo baada ya kufikisha alama 10.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited