Home Makala Man United Yashinda 3-0

Man United Yashinda 3-0

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya klabu ya Bentford katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliofanyika katika uwanja wa Brentford Community mjini Brentford, Middlesex.

Katika mchezo huo mabao ya Man utd yalifungwa na wachezaji waliopitia katika akademi ya klabu hiyo wakiongozwa na Marcus Rashford ambao aliyenza kufunga ni Anthony Elanga dakika ya 55, Mason Greenwood dakika ya 62 na Marcus Rashford dakika ya 77 akimaliza ukame wa mabao uliomuandama kwa muda mrefu, wakati bao pekee la Brentford limefungwa na Ivan Toney dakika ya 85.

Kutokana na ushindi huo ugenini sasa Man utd imefikisha jumla ya alama 35 ikicheza michezo 21 huku ikisalia nafasi ya saba ikizidiwa wastani wa mabao tu na Arsenal ambayo pia mechi moja mkononi, wakati Brentford inabaki na pointi zake 23 za mechi 22 katika nafasi ya 14.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited