Home Soka Yanga sc,Polisi Kukipiga Arusha

Yanga sc,Polisi Kukipiga Arusha

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Polisi Tanzania imethibitisha kuuhamisha mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Yanga sc kutoka katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi mpaka katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ulioko jijini Arusha kutokana na uwanja wa Ushirika kuwa na matumizi ya Serikali.

Awali kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu ilionyesha kuwa uwanja huo utatumika kwa mchezo huo mpaka hivi leo ilivyotoka taarifa rasmi ya kuwa na matumizi mengine ya kiserikali yatafanyika katika uwanja huo huku taarifa za ndani zikidai kuwa sababu kuu ni kufanyika kwa Tamasha la utamaduni ndio sababu kuu ya kuhamisha mchezo huo.

Wadau wengi wa soka nchini wanausubiri mchezo huo kwa hamu kubwa kutokana na rekodi ya Yanga sc ya kutopata ushindi mkoani ikicheza dhdi ya Polisi Tanzania ambapo mara nyingi imekua ikipata sare.

banner

Yanga sc imekua na msimu mzuri wa ligi kuu nchini ikishinda michezo kumi na kutoa sare miwili kati ya michezo 12 iliyocheza mpaka sasa huku Polisi Tanzania wao wakishinda michezo mitatu ya awali huku tisa iliyofuatia wakitoa sare ama kupoteza kabisa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited