Chicago Bulls imetangaza kuwa wamekabidhi mkataba wa nyongeza ya muda mrefu kwa kocha wao wa mkuu Billy Donovan kutokana na kazi njema aliyoifanya klabuni hapo kwa msimu ulioisha.
“Billy ni mwenye ujuzi na uwezo mkubwa wa kuongoza,” alisema Makamu wa Rais wa Bulls, Arturas Karnisovas. “Tunaamini kuwa ana uwezo wa kuleta mafanikio kwa timu yetu kwa miaka ijayo.”Alimalizia kusema bosi huyo mwenye ushawishi klabuni hapo.
Donovan alijiunga na Bulls mwaka 2020, na kwa sasa ameongoza timu kwa msimu wa pili mfululizo wa playoffs ambapo alinukuriwa akisema yafuatayo baada ya kusaini mkataba huo mpya ambao haujafahamika ni wa muda gani.
“Ninashukuru familia ya Bulls kwa imani yao,” alisema Donovan. “Nina hamu ya kuendelea kufanya kazi na wachezaji wetu wa kipekee na wataalamu wa klabu hii.”Alisema kwa hisia kali.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Bulls wameanza msimu wa 2023-24 kwa rekodi nzuri, na wanaamini kuwa Donovan ataendelea kuwaongoza kwenye mashindano ya juu.