Site icon Sports Leo

1.5B Kumng’oa Ahou Msimbazi

Klabu ya Simba Sc imesisitiza kuwa haiko tayari kumuachia kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua kwa dau chini ya shilingi bilioni 1.5 za kitanzania.

Awali klabu hiyo iliwasiliana na Kaizer Chiefs kuwa haitamuuza kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua (23) kutokana na kocha Fadlu Davis kuwa katika mipango yake ya msimu ujao.

Hata hivyo sasa hivi mabosi wa timu hiyo wapo tayari kurudi mezani ikiwa anayemuhitaji Jean Ahoua aweke USD 600K (Tshs 1.5 Bilioni) ili kumuachia mchezaji huyo ambapo itakua na uhakika wa kupata kiungo mwingine sokoni.

Kaizer Chiefs inavutiwa na inamfatilia kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua ambaye amekuwa na msimu bora sana akiwa na klabu hiyo akiongoza katika safu ya wafungaji bora mpaka sasa.

Exit mobile version