15
Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imeanza kutekeleza maelekezo ya Rais John Magufuli wa kubadili jina la Uwanja wa Taifa na kuwa Mkapa Stadium katika kumuenzi rais mstaafu wa awamu ya tatu, hayati Benjamin Wiliam Mkapa.
Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara hiyo, Yusufu Singo ameeleza kuwa mchakato umeshaanza na wameshaliondoa jina la zamani ili kuweka jina la Mkapa, kwa maelekezo ya Waziri wa Michezo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Rais Magufuli alitoa maelekezo ya kubadili jina la uwanja wa Taifa uitwe Uwanja wa Mkapa (Mkapa Stadium)wakati akitoa salamu za rambirambi kwenye kuuaga mwili wa  Mkapa, Jumanne hii kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.