Kiungo Mshambuliaji Dickson Ambundo ametua Dar usiku wa kuamkia leo kuja kuungana na klabu ya Yanga sc na kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa klabu hiyo baada ya kufikia makubaliano ya usajili muda mrefu.
Ambundo alikua mchezaji wa klabu ya Dodoma Jiji Fc na taarifa zinadai alishamalizana na klabu ya Yanga sc na ikibaki hatua ya utambulisho tu.
Tayari mchezaji huyo amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji watakaocheza michuano ya Kagame ambapo Yanga sc itashuka uwanjani leo kuumana na Nyasa Big Bullets.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.