Sports Leo

Assink Kumrithi Yao Kouassi

Makubalino yamefanyika baina ya klabu ya Yanga sc na Singida Black Stars ambapo sasa beki wa kati raia wa Ghana Frank Assink atajiunga na Klabu ya Yanga SC akitokea Singida Black Stars kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Mlinzi huyo anategemea kuwasili Tanzania muda wowote kuanzia leo huku ikiamuriwa kuwa mlinzi Yao Kouassi ataondolewa kwenye mfumo kwa sasa na badala yake beki huyo mpya ataingizwa ili kukamilisha idadi ya wachezaji 12 wa Kigeni wanaohitajika kwa mujibu wa kanuni.

Assink Kusajiliwa Yanga sc-Sportsleo.co.tz

Mabosi wa klabu ya Yanga sc wamefikia uamuzi huo kutokana na Yao kuwa na majeraha ambapo sasa anakaribia kupona lakini itamchukua miezi minne kuanzia sasa ili kuanza kucheza mpira katika hali ya mashindani ambapo kwa sasa anaendelea kufanya mazoezi maalumu ya kurejea uwanjani.

Assink ana uwezo wa kucheza nafasi ya beki wa kati pamoja na pembeni upande wa kulia hivyo Yanga sc wameona ni mbadala sahihi wa Yao Yao ambapo atakua akishirikiana na Israel Mwenda na Kibwana Shomari kuleta raha kwa wananchi upande huo wa kulia.

Pia kwa upande wa mabeki wa kati ataungana na Ibrahim Hamad na Dickson Job pamoja na Bakari Mwamnyeto ambapo atakua na kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa anapata namba mbele ya Job na Bacca ambao mpaka sasa wamekosa mpinzani kikosini humo kutokana na kuwa tayari na uhakika wa kuanza.

Tayari Yanga sc ilishakamilisha usajili wa mastaa kama Moussa Balla Conte,Lassine Kouma,Mohamed Hussein,Mohamed Doumbia,Celestine Eccua,Andy Boyeli,Abubakari Othman Ninju,Abdulnassir Mohamed Casemiro na Offen Chikola ambao wanatarajiwa kuleta ushindani kikosini humo kuelekea msimu ujao.

Exit mobile version