Home Makala Aston Villa Waipa Kichapo Watford

Aston Villa Waipa Kichapo Watford

by Sports Leo
0 comments

Timu ya  Uingereza Aston Villa imewapa kichapo Watford cha mabao 2-1 katika uwanja wa Villa Park huku mchezo ukisimamiwa na refa kutoka England Martin Atkinson.

Watford walianza kujipatia bao la kwanza dakika ya 38 kupitia Troy Deeney huku bao la kusawazisha kwa timu ya Aston Villa lilipatikana kipindi cha pili cha mchezo kupitia  Douglaz Luiz dakika ya 68.

Tyrone Mings aliongeza bao la pili kwa timu ya Aston Villa dakika ya 90 na kabla ya kipenga kulia alipokea kadi ya njano kutokana na kushangilia nje ya uwanja kabla ya mchezo kuisha.

banner

Aston Villa ikiwa nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza inakuwa imecheza jumla ya mechi 24 ikiwa imeshinda mechi 7 na kutoa sare mechi 4.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited