Mshambuliaji Pierre Emerick Aubameyang ameifanya Arsenal kutwaa ubingwa wa kombe la FA mara ya 14 baada ya kuwafunga Chelsea mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA kwenye uwanja wa Wembley.
Chelsea walianza kupata bao la kwanza dakika ya tano kupitia Christian Pulisic ambaye alishindwa kumaliza dakika 90 za mchezo kutokana na kupata majeraha.
Arsenal walisawazisha bao hilo kupitia Aubameyang dakika ya 23 kwa mkwaju wa penalti huku bao la pili kutoka kwa raia huyo wa Gabon lilifungwa dakika ya 67.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Chelsea walimaliza mchezo wakiwa pungufu kwani Mateo Kovacc alionyeshwa kadi za njano mbili na mwamuzi Anthony Taylor akifuatiwa na nyekundu baada ya kucheza rafu.