Home Makala Aubameyang Kutua Real Madrid Ni Ahadi

Aubameyang Kutua Real Madrid Ni Ahadi

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyanga amewapa mashabiki wa Arsenal kidokezi kuwa muda wake wa kuhudumu tena Emirates umekaribia kufika tamati kwa kuwa anatawaliwa na kiu ya kutimiza ahadi ya kucheza Real Madrid kwa kuwa ndio maneno ya mwisho aliyomuahidi marehemu babu yake kabla ya kuaga dunia.

Aubameyang alijiunga na Arsenal mnamo January 2018 na anajivunia kupachika wavuni jumla ya mabao 49 kutokana na mechi 75 zilizopita ,hadi kufikia msimu huu ametikisa nyavu za wapinzani mara 17 na ni miongoni mwa wafumaji wanaopigiwa tena upatu wa kutwaa taji la mfungaji bora Epl.

“Kabla ya babu yangu kuaga dunia miaka miwili iliyopita,nilimuahidi kwamba nitakuja kuwachezea Real Madrid siku moja na yeye alikuwa mzawa wa Avila ,mji mdogo uliopo karibu na Madrid ,Uhispania”alisema Aubameyang

banner

Aliongeza kuwa anajua hayatakuwa maamuzi rahisi ila anahisi kwamba hatopata kabisa utulivu iwapo atakataa kutimiza ahadi hiyo aliyotoa na itakuwa vibaya kusalia kudaiwa na nafsi yangu siku zote za maisha haya.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited