Klabu ya Azam Fc imezidi kujiwekea mazingira magumu ya kujinyakulia taji la ligi kuu nchini baada ya kulazimishwa suluhu na klabu ya Tabora United katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
Azam Fc iliyoanza bila mshambuliaji wake Prince Dube ilikua na wakati mgumu kupata nafasi ya kuipenya safu ya ulinzi wa Tabora United iliyokua chini ya beki kisiki Rajabu Zahir ambaye aliwadhibiti washambuliaji wa Azam Fc akianza na Abdul Sopu kisha Dube ambaye alingia kipindi cha pili.
Mpaka mpira unaisha Azam Fc haikupiga shuti lolote lililolenga lango licha ya kumiliki mpira kwa asilimia kubwa katika mchezo huo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kutokana na sare hiyo sasa Azam Fc imekua katika nafasi ya pili ya msimamo ikiwa na alama 36 huku Yanga sc ikiwa kileleni mwa msimamo na alama 43 huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 16 ya ligi kuu ya Nbc.