Azam Fc iliyochini ya kocha mkuu Arstica Cioaba ambaye pia ni raia wa Romania inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC leo majira ya saa 1:00 usiku katika uwanja wao uliopo Chamazi,Azam Complex.
KMC ilikuwa na mchezo wa kirafiki jana na Simba Sc Uwanja wa Uhuru ambapo ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1 hivyo leo watacheza mchezo wa pili na Azam Fc ambao waliwapiga mabao 2-1 Namungo Fc kwenye mchezo wa kirafiki siku ya Azam Festival.
Lengo la mchezo wa leo ni kujiweka sawa kwa ajili ya ligi kuu bara inayotarajiwa kuanza Septemba 6 ambapo Azam Fc watafungua pazia na klabu ya Polisi Tanzania.