Kikosi cha Azam Fc tayari kimeshatia nanga makao makuu ya nchi ,mkoani Dodoma kwa ajili ya mchezo wao wa kesho dhidi ya JKT Tanzania.
Mabingwa hao watetezi walinyooshwa na Namungo katika uwanja wa Majaliwa kwa kupigwa bao 1-0 katika mechi yao ya mwisho.
Katika msimamo wa ligi kuu bara Azam Fc ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi 24 kwa pointi 45 huku JKT Tanzania ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 38 kibindoni