Uongozi wa Azam Fc umeahidi kufanya tofauti msimu wa 2020/21 baada ya kuwa na msimu mbovu 2019/20 kwani wanaamini katika majembe ya kazi waliyoyasajili katika dirisha la pili la usajili lililofunguliwa Agosti mosi na kufungwa Agosti 31.
Azam FC inayonolewa na kocha mkuu,Aristica Cioaba ilikwama kutwaa taji 20219/2020 ikiwa ni pamoja na lile la Mapinduzi Cup, Kombe la Shirikisho, Kombe la Kagame pamoja na ubingwa wa ligi kuu bara.
Jambo hilo limewapa somo matajiri hao wa Dar es Salaam wenye makazi yao Chamazi na wapo tayari kutwaa ubingwa kwani wachezaji waliowasajili ni wenye uwezo mkubwa kwenye ushindani wa soka.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Wachezaji wapya wa Azam Fc ni Prince Dube, Awesu Awesu Pamoja na David Kissu hao watajumuika na wenzao kuvaana na Polisi Tanzania Jumatatu ya Septemba,7.