Home Makala Azam Fc Waifunga 2-0 Mbuni Fc

Azam Fc Waifunga 2-0 Mbuni Fc

by Sports Leo
0 comments

Ikiwa katika michezo ya kukiweka timamu kikosi hicho klabu ya Azam Fc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mbuni Fc ya jijini Arusha katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini humo.

Mabao ya Azam Fc yalifungwa na  Lusajo Mwaikenda kwa kichwa na Prince Dube huku wakifanikiwa kuonyesha kandanda safi mwanzo mpaka mwisho mwa mchezo huo uliokuwa wa kusisimua kwa pande zote mbili.

Azam Fc inajiandaa na ligi kuu nchini pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho la Azam Fc baada ya kutolewa katika michuano ya kimataifa ya kombe la shirikisho baada ya kutolewa na klabu ya Bahir Dar  Kanema ya nchini Ethiopia.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited